Tessera yo Lejio Maria
SALA ZA MWANZO
Kwa jina la Baba .......
Uje Roho Mtakatifu, uzienee roho za waumini wako, uwatie mapendo yako.
V. Peleka Roho yako, vitaumbwa vipya.
R. Na nchi itageuka.
Tuombe: Mungu Baba yetu, Shush mapaj i ya Roho wako Mtakatifu dun iani kote. Ulimtuma Roho kwa Kanisa lako kuanzisha mafundisho ya habari njema: twaomba huyu Roho azidi kufanya kazi uiimwenguni kupitia nyoyo za wote wanaoamini. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina.

V. Wewe, Bwana wangu utafungua mdomo wangu.
R. Na ulimi wangu utakusifu.
V. Mungu kunbuka kunisaidia.
R. Unisaidie sasa hivi.
V. Atukuzwe Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu.
R. Kama mwanzo na sasa na siku zote na milele. Amina.
Halafu yanafuata makumi matano ya Rosari na Salamu Malkia.
Salamu Malkia Mama mwenye huruma; Salamu kwako twapata uzima, ndiwe mwenye kutuletea kitulizo. Ndiwe ambaye tunakutumainia sisi wana maskini wa Hawa. Twakungoja kwa kulia na kulalamika chini hapa kwenye machozi. Haya basi, mwombezi wetu, utuelekezee macho yako kwa huruma. Tutakapotoka ugenini hapa, tufanyizie twende kumwangalia Yesu, mzao mbarikiwa wa tumbo lako. Ee Bikira Maria mwenye hururna, Ee Bikira mwema, Ee Bikira mpole.
V. Utuombee, Mzazi Mtakatifu wa Mungu.
R. Tujaliwe ahadi za Kristo.
Tuombe: Ee Mungu, ambaye Mwanao wa pekee ametupatia Ukombozi milele kwa kuzaliwa, kufa na kufufuka kwake; twaomba utufanyizie sisi tuliofikiri juu ya matendo hayo ya Rosari Takatifu, tupate nguvu za kufuata mafundisho vote yaliyomo na kupewa maagano yake kwa nj ia ya Kristo Bwana wetu. Amina.
V. Moyo Mtakatifu wa Yesu R. Utuhurumie.
V. Moyo wa Maria wenye usaf R. Utuombee.
V. Yosefu Mtakatifu R. Utuombee.
V. Yohani Mwinjili Mtakatifu R. Utuombee.
V. Ludoviko Mtakatifu wa Montfort R. Utuombee.
Kwajina la Baba.....
KATENA YA LEJIO

Antiphonu. Nam huyu binti atokaye kama
alfajiri, mzuri kama mwezi, ana nuru kama jua, anatisha kamajeshi lililo tayari kupigana?
+ Moyo wangu wamtukuza Bwana.
Na Roho yangu imeshangilia katika Mungu
Mkombozi wangu.
Kwa kuwa ameuangalia unyenyekevu wa
mtumishi wake; toka sasa vizazi vyote watanisifu
mwenye heri.
Kwani amenitendea makubwa aliye Mwenyezi,
na jina lake takatifu.
Na huruma yake ipo toka kizazi hata kizazi
kwa wale wenye kumcha.
Ameonyesha enzi kwa mkono wake.
amewatawanya wenye kiburi mioyoni mwao.
Amewaondosha wenye enzi katika kiti,
akawakuza wanyenyekevu.
Wenye njaa amewashibisha mema,
matajiri akawarudisha mikono mitupu.
Amempokea lsreal mtumishi wake,
akikumbuka huruma yake.
Kama alivyowaambia baba zetu;
Ibrahimu na wazao wake hata rnilele.
Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.
Kama mwanzo na sasa na siku zote na milele.
Amina
Antiphonu. Nam huyu binti atokaye kama
alfajiri, mzuri kama mwezi, ana nuru kama jua, anatisha kamajeshi lililo tayari kupigana?
V. Ee Maria uliyeumbwa pasipo dhambi ya asili.
R. Utuombee sisi wenye kukimbilia kwako.
Tuombe: Ee Bwana Yesu Kristo, uliye mpatanishi wetu kwa Mungu Baba na uliyekubali kumteua Mama yako Bikira Maria kuwa Mama yetu, pia na Mpatanishi wetu kwako, tunakuomba kila anayekuja kuomba wema wako umjalie na afurahi kuupokea kwa kupitia kwake. Amina.

SALA ZA MWISHO

Kwa jina la Baba .....
Tunakimbilia ulinzi wako Mzazi
Mtakatifu wa Mungu, usitunyime tukiomba katika shida zetu, utuokoe siku zote tuingiapo hatarini, ewe Bikira mtukufu mwenye baraka.
Amina.

V. Maria uliyekingiwa dhambi ya asili, mtoaji
wa neeroa zote
(au Jina la Praesidium) R. Utuowbee
V. Mach Mtakatiful, na Gabriel Mtakatifu R. Mtuombee
V. Enyi nguvu za mbinguni Malaika wa Jeshi
la Maria R. Mtuombee.
V. Yohani Mbatizaji Mtakatifu R. Mtuombee.
V. Petro na Paulo Watakatifu R. Mtuombee.
Ee Mungu Mwenvezi utuanUalie sisi tnlioingia katika Legio ya Maria, utujaze na moyo wa imani kwako na kumtunaini yeye ili tuweze kuishinda dunia. Tia ndani ya nyoyo zetu imani kuu pamoja na mapendo kusudi ya kufanya kazi zetu zote kwa ajili yako tu, na kumpenda jirani yetu kabisa na kumsaidia pia kwa ajili yako. Tunaomba imani iliyo imara kama jabali isiyoweza kushindwa na matata ya dunia hii, au na mashaka mengine yote. Tunaomba imani kuu itakayotupa nguvu ya kumaliza mambo makubwa kwa ajili ya utukufu wako na kwa wokovu wa roho za wengineo. Tunaomba imani yenye kutuongoza kwa umoja, tukiwasha kila mahali moto wa mapendo yako, kuwasaidia watu walio gizani na wakaao ndani ya kivuli cha mauti, kuwapa nguvu wale wengine wanaotaka kulegea nao waliotenda dhambi kubwa kuwarudishia uzima. Tunaomba neema ya kutuongoza sisi wenyewe katika njia ya amani ili mwisho wa dunia, sisi sote tulio katika Lejio ya Maria tuingie ufalme wa Mungu wenye utukufu milele. Amina

Roho za marehemu Walejio wetu, pamoja na roho za maoehernu wote, wapumzike kwa amani. Arnina:
Kwa jina la I3aba .......
(Kiswahili)
Cum Permissu Superiorum